SMS kwa matukio, harusi na waandaaji wa matukio
Alika wageni, kusanya michango na shiriki mabadiliko ya dakika za mwisho ndani ya dakika chache. GetSMS inasaidia waandaaji wa matukio, kamati za harusi, waandaaji wa mikutano na kumbi kuwafikia wageni wote kwa SMS.
Kwa nini waandaaji wa matukio hutumia SMS
Mawasiliano ya tukio yanaendeshwa na muda: mialiko, michango, tarehe za kuthibitisha, mabadiliko ya ukumbi na vikumbusho siku ya tukio. SMS inamfikia kila mgeni bila kujali aina ya simu, na kampeni moja inaweza kwenda kwa mamia ya watu kwa wakati mmoja.
Kamati za harusi na send-off Tanzania hutumia SMS kualika wanakamati kwenye vikao vya michango, kuwakumbusha waliotoa ahadi na kushiriki ratiba ya programu. Ujumbe wa kibinafsi kutoka orodha ya Excel unaweza kujumuisha jina la kila mgeni na kiasi cha ahadi.
Waandaaji wa mikutano na matukio ya kampuni hutumia SMS kwa uthibitisho wa usajili, mabadiliko ya ratiba na maelekezo ya njia, na hupanga vikumbusho mapema ili vitumwe kwa wakati sahihi.
Unachoweza kutuma
- Mialiko ya harusi, send-off na kitchen party.
- Taarifa za vikao vya michango na reminders za ahadi.
- Uthibitisho wa usajili wa mikutano na warsha.
- Taarifa za ukumbi, mavazi na programu.
- reminders za siku ya tukio na mabadiliko ya dakika za mwisho.
- Ujumbe wa shukrani baada ya tukio.
Mifano ya ujumbe
Ndugu Musa, tunakukumbusha ahadi yako ya TZS 100,000 kwa harusi ya John na Grace. Kikao kijacho ni Jumamosi saa 10 jioni, Ubungo. Asante.
Herufi 137
Kikumbusho: Tech Summit inaanza kesho saa 2:30 asubuhi ukumbi wa Mlimani City. Kuja na namba yako ya usajili DT-4412 kwa kuingia. Tunakusubiri!
Herufi 143
Jinsi GetSMS inavyosaidia waandaaji wa matukio
Panga mapema
Andika vikumbusho mara moja na uvipange kwa siku na saa sahihi, ili hakuna kinachotegemea mtu kukumbuka kubonyeza kutuma.
Mialiko ya kibinafsi
Ingiza orodha ya wageni kutoka Excel na uweke jina la kila mgeni, meza au kiasi cha ahadi kwenye ujumbe.
Taarifa za papo hapo
Ukumbi au muda ukibadilika, kila mgeni anapata taarifa ndani ya dakika chache, si baada ya msururu wa simu.
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
Je, naweza kutuma Reminders za Michango ya harusi kwa SMS?
Ndiyo. Ingiza orodha ya waliotoa ahadi pamoja na majina na kiasi kutoka Excel na umtumie kila mtu kikumbusho cha kibinafsi. Kamati nyingi hutuma kikumbusho kimoja kabla ya kila kikao cha michango.
Je, ninahitaji kampuni ili kutumia GetSMS kwa tukio?
Hapana. Watu binafsi na kamati wanaweza kujisajili, kununua kifurushi kidogo cha salio kwa pesa ya simu na kutuma kutoka dashibodi. Unaweza kuanza na mtumaji wa kawaida wa GetSMS au kuomba Sender ID yako.
Je, naweza kupanga kikumbusho cha asubuhi ya tukio?
Ndiyo. Chagua tarehe na saa unapotengeneza kampeni na GetSMS itatuma kiotomatiki.
Suluhisho zinazohusiana
Anza kuwafikia wateja wako kwa SMS leo
Usajili ni bure na unajumuisha SMS 5 za majaribio. Nunua salio zaidi kwa pesa ya simu wakati wowote.